Uvira all stars – Karibu Uvira, uva-unit:

http://www.youtube.com/watch?v=HAO0eJ27fUE&feature=share

Hawa ni vijana wa Uvira (Sud-Kivu/DRC). Waza hawa vijana gisi wanavyo perform, wangepata uwezo napesa za kuendeleza kazi ya uimbaji? Wanaonyesha kama vijana wana uwezo wa kuyigeuza inchi ya vita na ubaguzi mara nyingi nakuyielekeza kwenye muelekeo muzuri wa maendeleo na kuishi pamoja. Ningefurahiya kuwaona vijana wengi wakiendeleza umaarufu wayo kwakuyielekeza inchi kwenye amani.
Wengine vijana kama hawa wamepoteleya kati yamakundi yenye silaha kabla wangefanya kazi mbali mbali kama hizi zinazowasaidiya kuendeleya. Ndiyo maana hawa waimbaji wanaomba viongozi kuijali Uvira. Munaziona barabara kwenye video zimebomolewa, hospitals zimeisha, masomo wazazi wanajilipiya, vijana wanakosa kazi na mengine kama hayo. Na siyo Uvira tu, fasi nyingi Kongo ni kama hivo. Kwanini viongozi wahawezi kuyigeuza hali hiyi? swali lakini sipati jibu haraka.
Ninachokiweza kama msaada nikuyiweka video hiyi kwenye blog.
Aksanti sana vijana wa UVIRA

[polldaddy poll=7990138]

About admin 430 Articles
PhD & Visiting researcher @POLISatLeeds. Interest: Microeconomic Analysis of Violent Conflict, Genocide Studies and violence targeting minority groups. Congolese, blogger advocating for Equitable Redistribution of Ressources & national wealth as well as & #Justice4All #DRC. On top of that, I'm proud of being a "villageois"

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*


This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.