Jeshi la Taifa la Congo, FARDC kuwasaka Maimai Yakutumba

Wakati ambapo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inajiandaa kufanya uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu wa 2018, kumeripotiwa mapambano mapya kati ya jeshi la taifa (FARDC) na kundi la Maimai maeneo ya Lulenge. Mapambano hayo yameripotiwa kuaanza tarehe 19 hadi 21 mwezi huu wa tatu tarafani FIZI, mukowa wa Kivu ya Kusini, Mashariki mwa Congo.

Siku chache zilizo pita, jeshi la taifa lilisambaratisha kundi hilo la Maimai inayojiita Yakotumba lililokuwa katika kisanga cha Ubwari. Mapambano hayo yame ripotiwa miezi mbili iliyo pita eneo hizo za Ubwari/Kazimia.

Shirika la raia (Societe Civile)maeneo ya Lulenge liliripoti kwamba kundi la Maimai bado liko hai katika maeneo hayo ya Lulenge na mwenyewe kiongozi wa kundi hilp akiwa sehemu hizo.

Jeshi la taifa linajitaidi kuzibiti makundi yote yanayo shikilia silaha kinyume cha sheria ili kuhakikisha uchaguzi inchini humo unafanyika katika usalama.

THOMSON UNDJI B. W.

Radio Tumaini/Tanganyika

About admin 459 Articles
PhD & Visiting researcher @POLISatLeeds, proud of being a "villageois". My interest: Peace, conflict, Genocide Studies, Minority ethnic groups, DRC, African Great Lakes region. Congolese, blogger & advocate #Justice4All in #DRC.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*


This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.