Wachimba madini wanaozaniwa kuwa ishirini (20) wasemekana kuwa wamepoteza maisha yawo hiyo jana, jumatatu 26/03/2018 huko Misisi, terriroire ya Fizi (Kivu ya Kusini).
Kwa mujibu wa viongozi wa serekali eneo hilo, ajali hiyo lilitokea katika migodi inayo itwa Ndende, na imetokana na mmomonyoko wa arzi ulio waangukiya wachimba madini.
Dudu zinazo aminika zinasema kwamba wiki iliopita, wachimba madini wengine wanasemekana kuwa wameuwawa kutokana nakubomoka kwa arzi tena vifusi.
Wana mazingira eneo ilo ueleza kua inakua hatari kila muhula wa kipindi mvua inyeshapo.
Inawezekana kuwa watu hawo wanaitaji msaada kutoka kwa serikali, zaidi sana ili kuhakikisha kuwa uchimbaji unaendeleshwa panapo kuwa na usalama wawachimbaji.
THOMSON UNDJI.
Radio Tumaini/Tanganyika
Leave a Reply